Full-Width Version (true/false)


TAARIFA KUHUSU KAMPENI YA "TUSHIKANE MIKONO"


Mtilah Blog imeanzisha kampeni ya kijamii ya kusaidia watu wanaohitaji misaada mbalimbali kama vile matibabu, masomo,waliopatwa na majanga, kusaidia yatima, kusaidia watu wenye mahitaji maalumu nk.

Kampeni hiyo amabayo imepewa jina la "Tushikane Mikono" inalenga kuwaunganisha watu wanaohitaji misaada na wananchi au mashirika ambayo yataweza kuwasaidia watu hao kutokana na matatizo yao.

Mtilah Blog imeona kwamba kuna watu wana shida za msingi na wanahitaji misaaada pia kuna watu wanaweza kusaidia wale wenye shidala kwa kile kidogo walichojaaliwa, hivyo Mtilah Blog itakuwa inaangalia watu wanaohitaji misaada  nakuwaonesha kwa jamii au wadau mbalimbali ili waweze kuwasaidiwa,

Kutoa ni moyo,Mungu ndiyo anaegawa riziki kwa kila kiumbe. Kumsaidia mtu siyo lazima uwe na maghorofa, Magari au maisha ya kifahari, ni chocho ambacho unaona ukimpa mwenzio kitamfaa.

Kumbuka kuna watu hata mlo mmoja kwa siku kwao ni shida,kuna mtoto yupo shule lakini anakosa vifaa vya shule kuna watu wanakosa nguo za kuvaa,kuna watu wanakosa matibabu kwa kushindwa kumudu gharama,Mtilah Blog kwa kuliona hilo imeamua kushirikiana na jamii ilikuweza kuunganisha makundi haya mawili.

Tushikane mikono kwa kile ambacho Mungu ametujaalia.Hakuna anaependa kuwa maskini,hakuna anaependa shida. Yote ni makadirio ya Mungu.

Mtilah Blog kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tutakuwa na kampeni za kutembelea wagonjwa,vituo vya watoto yatima,kutembelea shuleni ,watoto wa mitaani  na makundi mengine ya watu ambao kwa uhalisia wanahitaji kushikwa mikono ili waweze kuendesha maisha ili waweze kufurahi,kuwa na amani kama wengine.

Sambamba na kutembelea sehemu hizo,pia mtu anaweza kutupatia taarifa ya mtu ambae ana shida ya msingi na anahitaji msaada ili tuweze kumuunganisha na wasamaria wema .Lakini pia kama mtu ana chochote  unahitaji  kusaidia unaweza kuwasiliana nasi ili tukuunganishe na wanaohitaji msaada huo. 

pia Kama una nguo ambazo huzivai,tunazikusanya ili kuwapatia wale wanaozihitaji.

Tunakaribisha wadau kuungana nasi kwa jambo hili .Kwa lolote lile wasiliana na Uongozi wa Mtilah Blog ambao ni waanzilishi wa kampeni hii kwa njia zifuatazo

Simu: 0658303252
           0625205937

Email: news@mtilah.com

"TUSHIKANE MIKONO"

No comments

Powered by Blogger.