Full-Width Version (true/false)


USIKUBALI KUPITWA NA TETESI HIZI MUHIMU ZA SOKA ULAYA.

Ronald Koeman looks dejected
Meneja wa Everton Ronald Koeman anakaribia kumwaga unga baada ya timu yake kulazwa 1-0 nyumbani na Burnley siku ya Jumapili. (Sun)
Mholanzi huyo amesema kwa sasa mustakabali wake katika Goodison Park haumo mikononi mwake tena. (Daily Mirror)
Naye Koeman amesema mshambuliaji Wayne Rooney, 31, bado alikuwa na "mtazamo mwema" licha ya kuachwa nje katika mechi hiyo ambayo walilazwa 1-0. (The Times)
Meneja wa West Ham Slaven Bilic atapewa muda wa hadi mwisho wa msimu kudhihirisha uwezo wake katika klabu hiyo. (Daily Mirror)
Everton nao inadaiwa hawatarejea tena kumtafuta mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, dirisha la kuhama wachezaji litakapofunguliwa tena mwezi Januari. (Daily Star)
Crystal Palace wanapanga kuwasilisha ombi la kumchukua mshambuliaji wa zamani wa AC Milan Alberto Gilardino. Mchezaji huyo wa miaka 35 hajajifunga kwenye mkataba wowote ule baada ya kuondoka Pescara. (ESPN)
Aston Villa nao wameendeleza juhudi za kutaka wamchukue mchezaji Sam Johnstone, 24, waliyekopeshwa na Manchester United kwa mkataba wa kudumu mwezi Januari. (Manchester Evening News).
Emmanuel Eboue
Meneja wa Villa Steve Bruce naye amesema kiungo wa kati Conor Hourihane, 26, hataondoka klabu hiyo iwapo klabu hiyo haitalipwa "pesa nyingi sana". (Birmingham Mail)
Mjasiriamali Amanda Staveley alikuwa St James' Park Jumapili huku tetesi zikiendelea kuenea kwamba huenda anataka kuinunua klabu ya Newcastle. (Sun)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, 29, amesema huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Telefoot, kupitia Calciomercato)
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham Carlton Cole, 33, anaweza kuhamia Crystal Palace iwapo klabu hiyo itamtaka. (Sky Sports)
Babake nyota wa Brazil Neymar, 25, alikuwa amemshauri kukataa uhamisho wake uliovunja rekodi ya dunia kwenda Paris St-Germain na badala yake asalie Barcelona. (Telefoot, kupitia Goal)
Afisa mkuu mtendaji wa Juventus Beppe Marotta amesema klabu hiyo ya Italia iliwasilisha dau ya kumtaka kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 23, majira ya joto lakini dau hiyo ikakataliwa. (Premium Sport, kupitia Calciomercato)
Mkufunzi mkuu wa Watford Marco Silva anasema aliishawishi bodi ya klabu hiyo kuidhinisha ununuzi wa chipukizi wa Brazil Richarlison mwenye umri wa miaka 20 majira ya joto. (Squawka)
Zlatan Ibrahimovic
Beki wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue, 34, anakusudia kufufua uchezaji wake katika klabu ya Turk Ocagi Limassol nchini Cyprus. (Sun)
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, naye amesema hana majuto yoyote kutokana na uamuzi wake wa kuihama Chelsea. (Guardian)
Difenda wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amesema klabu hiyo haikutumia fursa ya dirisha la kuhama wachezaji kutatua baadhi ya matatizo kwenye kikosi chao. Amesema hatarajii klabu hiyo ipiganie taji la ligi. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 35, anapata nafuu vyema, daktari aliyemfanyia upasuaji baada yake kupata jeraha la goti amesema. Hata hivyo, hataharakishwa kurejea kucheza. (Manchester Evening News)
Birmingham City wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Crystal Palace Jonny Williams, 23, aliye kwa mkopo Sunderland. (Birmingham Mail).

No comments

Powered by Blogger.