Full-Width Version (true/false)


Abiria wa mwendokasi wagoma Kimara
Leo May 7, 2017 katika kituo cha mabasi ya mwendokasi cha Kimara Mwisho, abiria wa mabasi hayo wamefanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuandamana kwenye njia ya mwendokasi.

Ayo TV na millardayo.com imefanya mawasiliano na shuhuda aliyekuwa eneo hilo Alexander Wencelaus ambaye ameeleza kuwa vurugu hizo zilisababishwa na uhaba wa magari hayo ya mwendokasi.

Ameeleza kuwa magari yote yaliyokuwa yanapita kituoni hapo yalikuwa yamejaa kiasi cha kutoweza kuchukua abiria wengine kwenye kituo hicho.

Baada ya changamoto hiyo kudumu kwa saa kadhaa ndipo abiria walipoanza kupita kwenye njia ya mwendokasi kwa ‘kuandamana’ wakishinikiza magari yaongezwe ili kutatua changamoto hiyo.

Hata hivyo baada ya muda changamoto hiyo ilitatuliwa kwa magari ya ‘Express’ kuanza kuchukua abiria kituoni hapo na hatimaye shughuli nyingine katika eneo hilo kuendelea kama kawaida.

No comments

Powered by Blogger.