Full-Width Version (true/false)


ACT wapingana na MagufuliChama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye siasa vyuoni kwa taratibu zilizowekwa kwa sababu vyuo ni kitovu cha mabadiliko ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwa chimbuko la viongozi mbalimbali.  
Wito huo umetolewa leo na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ambapo amekinzana na kauli ya Rais  Magufuli aliyoitoa siku chache alipotembelea Chuo cha Kilimo cha Sokoine kuwataka wanafunzi wasifanye siasa vyuoni.

Kiongozi huyo amesema "Kupiga marufuku siasa vyuoni ni kujenga taifa la vijana waoga, wasiokuwa na uwezo wa kuhoji.  Vijana msiache kuhoji mambo ya msingi kwa jamii zenu, hiyo ndiyo maana ya usomi" na kwamba maisha ya siasa wakiwa vyuoni ndiyo yaliwapa ujasiri wa kuingia kwenye ulingo wa siasa. 

Mbali na hayo Chama hicho kimeshauri kuwepo kwa mfumo mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kutokana na mfumo uliopo sasa kutokidhi mahitaji ya wanafunzi hali inayopelekea wengi wao kukosa mikopo.

No comments

Powered by Blogger.