Full-Width Version (true/false)


Adam salamba na Habib kiyombo kutua Azam FcIkiwa tunaelekea mwishoni mwa msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara VPL,baaddhi ya timu zimeanza kujianda na msimu ujao kwa kusajili wachezaji wapya.

Tetesi kutoka chanzo kinachoaminika zinasema kuwa klabu ya  imefanya mazungumzo na mastraika wawili,Adam salamba wa Lipuli Fc na Habib kiyombo wa Mbao FC.

Mmoja wa wajumbe wa bodi ya azam ,Nassoro Idrisa amesema msimu huu walipata tabu katika kupata mabao baada ya washambuliaji wao kushindwa kufunga mara kwa mara jambo ambalo alisema hawatataka litokee msimu ujao.

Azam ambayo inashika nafasi ya pili imefanikiwa kufunga mabao 32 mpaka hivi sasa huku Simba inayoshika nafasi ya kwanza ikiwa imefunga 61, jambo ambalo limewakera mabosi wa timu hiyo na kuamua kusaka mastraika wa maana sokoni.

No comments

Powered by Blogger.