Full-Width Version (true/false)


Alichokizungumza Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Nje wa UjerumaniMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas.Makamu wa Rais amesema kwa pamoja wamekubaliana kusaidiana katika kuleta utaalamu na teknolojia kwenye viwanda vya Tanzania haswa kwenye maeneo ya Kilimo, Uchimbaji Madini na Viwanda vya Madawa.

Makamu wa Rais asema Tanzania na Ujerumani wana Historia ya miaka mingi hivyo wamekubalina pia kujenga uwezo kwenye mambo ya uhifadhi ili kuvumbua mambo zaidi ambayo yapo Tanzania ili kukuza Utalii wa kuonyesha mambo ya Tanzania na Historia yake.

Makamu wa Rais amewashukuru kwa msaada wa masuala ya Afya haswa Afya ya Mama na Mtoto pamoja na uendelezaji wa shughuli za Utalii.

Makamu wa Rais aliwaomba wasaidiane katika kuzalisha umeme zaidi hapa Tanzania na kuwataka kuleta wawekezaji Zaidi Tanzania na wamekubalina hayo.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,Heiko Maas alisema amefurahi kutembelea Tanzania na ameisifia ni nchi nzuri sana na kuahidi kuendelea kwa Ushirikiano pamoja na kuendelea kusaidia katika masuala mbali mbali ya kuleta maendeleo.

Katika Mkutano huo , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Gavu walihudhuria.

Tazama picha Zaidi;
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments

Powered by Blogger.