Full-Width Version (true/false)


Alikiba Aeleza kwa nini hana mlinzi (BodyGuard), "Kama wewe ni mwema kwa nini utembee kwa wasiwasi?"Msanii wa bongo fleva Alikiba leo hii May 11,2018 amefunguka na kueleza kwa nini yeye hatembei na mlinzi "BodyGuard"

Wakati akihojiwa na kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na clouds Tv,Alikiba ameeleza kwamba binadamu yeyote aliye mwema amekamilika na hana maasi hawezi kuwa na wasiwasi wa kutembea na walinzi kwa sababu ana uhuru wa kwenda sehemu yeyote bila shida,na ndivyo ilivo kwake.

 "Binaadamu yeyote aliye kamili, aliye mwema ana uhuru wa kutembea kwa kujiamini kwenye ardhi ya Mwenyezi MUNGU. Kama wewe ni mwema, hujatenda maasi kwa nini utembee kwa wasiwasi?". Alisema alalikiba na kusisitiza kwamba anaamini mashabiki wake ndio watu wake wa karibu zaidi na humtazama popote alipo.

Siku ya leo Clouds Fm na Tv wanaiita Alikiba day kwa sababu wameamua kifanya mahojiano. na msanii huyo  kuanzia asubuhi hadi jioni kuanzia kipindi cha clouds 360,Leo tena,Xxl,Jahazi,Amplifaya na baadae kumaliza na Shilawadu ambapo kupitia mahojiano hayo alikiba atapata fursa ya kutambulisha kinywaji chake kiPya cha Mofaya pia kutambulisha wimbo wake mpya.

Mtilah Blog tutakujulisha kila kinachoendelea

No comments

Powered by Blogger.