Full-Width Version (true/false)


Alikiba aomba msaada kwa watanzaniaMsanii wa Bongo Fleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba a.k.a King kiba amefunguka na kuwaomba watanzania wanaopenda soka nchini Tanzania kiujumla wamchagulie kikosi bora wanachokikubali kutoka katika timu tofauti kwenye ligi kuu. 
Alikiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimebaki siku chache kuelekea mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Juni 9, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo lengo kubwa la mchezo huo ni kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na ujenzi wa miundombinu mashuleni. 

"Kwa kutambua umuhimu wa elimu nchini nimeamua kuwa balozi wa kujitolea na siku ya Juni 9 nitacheza mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na ujenzi wa miundombinu mashuleni. Tukutane Taifa naomba unichagulie kikosi bora unacho kikubali kutoka timu tofauti katika ligi ya Tanzania Bara", amesema King Kiba.

Katika mchezo huo wa kirafiki Alikiba anatarajiwa kuwa nahodha wa kikosi ambacho atasaidiwa kuchaguliwa na 'followers' wake wa mitandao ya kijamii pamoja na wale wanaoshabikia muziki wake wa bongo fleva na wengine.

No comments

Powered by Blogger.