Full-Width Version (true/false)


Alikiba Avunja Ukimya Kuhusu Kutomtaja Baba yake Katika Mafanikio yake Kwenye Muziki

Msanii wa Bongo Fleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba amefunguka na kudai sababu kubwa ya yeye kuwa anamtaja mama yake mzazi kila mara ni kutokana na kumpa ushirikiano mkubwa katika kukikuza kipaji chake cha kuimba kuliko baba yake mzazi kwasababu alikuwa mtu wa kusafiri sana.

 Alikiba ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ndani ya Heshima ya BongoFleva inayorushwa mubashara kupitia EATV baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho kuwa ni kwanini kila mara anapenda kumzungumzia mama na sio baba.

"Baba yangu kiukweli alikuwa ni international driver, alikuwa anasafiri mara kwa mara nchi tofauti tofauti yaani kachafua bara la Afrika zima. kwa hivyo alikuwa yupo busy sana muda mwingine alikuwa anaweza kukaa nje ya nchi hata mwezi mmoja au hata mitatu", amesema Alikiba.

No comments

Powered by Blogger.