" Alikiba naomba wahurumie" - Ommy Dimpoz
Ommy
Dimpoz alisema hayo baada ya Alikiba kutangaza rasmi kuwa wimbo huo
mpya wa Ommy Dimpoz ukifikisha watazamaji milioni tatu Youtube basi na
yeye ataamsha dude na kuachia wimbo wake mpya baada ya 'Seduce Me'
ambayo iliachiwa mwaka jana mwezi Agosti.
Baada ya ahadi hiyo ya Alikiba ndipo alipokuja Ommy Dimpoz na
kumuuliza Alikiba kama atatoa ngoma zote tano kwa wakati mmoja au
ataanza kuachia moja moja, hii ni ishara kwamba tayari kuna nyimbo zaidi
ya tano kutoka wa Alikiba ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa.
Aidha Msanii Alikiba akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki yake
kupitia mtandao wa jamii ambaye alitaka kufahamu kuwa hilo dude
ataliamsha lini ndipo alipojibu kuwa anawapa siku 10 tu baada ya hapo
anaweza kuachia wimbo wake huo mpya.
No comments