Full-Width Version (true/false)


Aliyeidanganya Yanga afungiwaShirikisho la soka nchini (TFF) kupitia kwa Kamati ya masaa 72 ya shirikisho hilo, imemfungia mchezaji wa Mbeya City Ramadhani Malima kwa kosa la kudanganya kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Mbeya City na Yanga. 
Kamati hiyo imemfungia Malima mechi tatu na faini ya laki tano kwa kosa la kuingia uwanjani kwa mara ya pili baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu wakati mchezo ukiendelea.

Mchezo huo uliopigwa April 22 kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, hivyo kuifanya Yanga kufikisha alama 48 ambazo imeshindwa kuziongeza jana baada ya kupata kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Prison kwenye uwanja huohuo.

Mechi hiyo ilichezeshwa na Shomari Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Omar Juma wa Dodoma na Godfrey Kihwili wa Arusha. Malima alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kumfuatia kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Yussuf Mhilu.
Hadi sasa Malima ameshatumikia mechi moja hivyo amebakiza mechi mbili katika adhabu yake hiyo. Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 48 huku Mbeya City ikishika nafasi ya 11 ikiwa na alama 29.

No comments

Powered by Blogger.