Full-Width Version (true/false)


Aliyemchora Tatoo Dogo Janja Kwapani Afunguka Gharama Yake

Msanii wa Bongofleva Dogo Janja aliamua kuonesha kuwa ana upendo wa dhati kwa mkewe Irene Uwoya baada ya kuamua kuchora tattoo yenye jina la Irene Uwoya katika mwili wake na kuamua kupost katika instagram account yake.

Mchoraji wa Tattoo hiyo ambaye anafahmika kwa jina la Testa Tattoo ambaye amehusika kwenye uchoraji wa Tatto za mastaa kama Wema Sepetu, Irene Uwoya na Wengine amezungumza gharama na jinsi alivyomshawishi Dogo Janja kubadili sehemu ya kuchorea Tattoo yake na kumshauri achore kwapani.

"Alinipigia simu akitaka kuchora  tatoo na tumetumia dakika 45 ambayo gharama yake ni laki moja na nusu mara ya kwanza alitaka kifuani ila nilimshauri kuchora pale nikamwambia huu ni mkono wa kumkumbatia mpenzi wake nilimshauri na aliupokea ushauri wangu" alisema  Mchora tatoo.

No comments

Powered by Blogger.