Full-Width Version (true/false)


Aliyeolewa mara 11 auawa na Al - Shabab

Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.
Shukri Abdullahi Warsame alishutumiwa kuolewa mara 11 bila kutalikiwa na waume zake waliopita.

Sehemu ya kiwiliwili chake kilifukiwa ardhini kichwa kikiachwa juu kisha akapigwa mawe na wanamgambo mjini Sablale mpaka umauti.

Mwaka 2014,wapiganaji wa al-Shabab walimpiga mwanamke mmoja na mawe baada ya kumshutumu kuolewa na wanaume wanne kwa siri, wilaya ya Barawe nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.