Full-Width Version (true/false)


Aliyetangaza kumnunulia Zari Range Rover Sport 2017 ala za uso

 

Zari The Boss Lady amesema hamfahamu Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya aliyetangaza kumnunulia mrembo huyo gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017.
Hapo jana Ringtone Apoko aliweka wazi kuwa amenunua gari hilo baada ya kusikia Zari atawasili nchini humo kwa ajili ya event yake, pia kipindi cha nyuma msanii huyo alipopata taarifa za Zari kuachana na Diamond alijitokeza na kueleza ana nia ya kumuoa.

Sasa leo May 11, 2018 Zari akiwa nchini Kenya amehojiwa na kituo cha Radio, Kiss FM na kueleza kuwa hamfahamu msanii huyo.

“Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi,” amesema Zari.

Zari yupo nchini Kenya kwa ajili ya even yake ‘The Colour Purple’ itakayofanyika weekend hii Uhuru Gardens.

No comments

Powered by Blogger.