Aliyetoroka kwa madai ya kuua mke, mtoto akamatwa
Tabora. Mkazi wa Kijiji cha Malema wilayani
Uyui mkoani Tabora, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mke wake na
mtoto kwa kuwachoma na kitu chenye ncha kali kutokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo
aliyetenda kosa hilo Mei 15 na kutokomea kusikojulikana alikamatwa juzi katika
Kijiji cha Tura wilayani Uyui.
“Baada
ya kuwaona askari polisi, mtuhumiwa alijaribu kujiua kwa kujichoma tumboni kwa
kisu lakini alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete
ambako anaendelea na matibabu akiwa chini ya ulinzi na hali yake inaendelea
vizuri,” alisema Kamanda Mtafungwa.
Akizungumzia
tukio la mauaji, alisema Mei 15, mtuhumiwa akiwa na nia ovu alimvizia mke wake,
Moshi Daud (24) na mwanaye Mohamed Matonya (mwaka mmoja) wakiwa wamelala na
kuwaua kwa kuwachoma na kitu chenye ncha kali.
“Inadaiwa
mtuhumiwa alikuwa akimhisi mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa
mashemeji zake,” alisema Kamanda Mutafungwa.
Mkoa
wa Tabora umekuwa na matukio kadhaa ya mauaji mengi chanzo chake kikuu ikidaiwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi, imani za ushirikina, kulipiza kisasi na ujambazi.
No comments