Full-Width Version (true/false)


Amber Lulu ataja list ya Mastaa aliotoka nao kimapenzi, ‘Aslay kiboko kabisa’

 

Sio ishu ya kawaida Bongo ila huwa inatokea, msanii Amber Lulu ametaja orodha ya mastaa ambao amewahi kutoka nao kimapenzi.
Muimbaji huyo anayetikisa na ngoma ‘Jini Kisirani’ katika orodha hiyo amejikuta akimsifia zaidi Aslay kuliko hao wengine.

“Barnaba, Aslay, Rammy Galis naYoung Dee lakini Young Dee sio sana, hao wanatosha, hao wengine hapana,” amesema.

“Aslay nilishatoka naye ila alikuwa ni mtu fulani muelewa, yuko poa, ana heshimu mwanamke. Yuko noma, yuko vizuri, Aslay kiboko kabisa,” Amber Lulu ameiambia Clouds TV.

Katika hatua nyingine Amber Lulu amesema kuwa mpenzi wake wa sasa, Prezzo amechukia sana kufuatia kuvuja kwa video yake chafu akiwa na msanii Nuh Mziwanda, hata hivyo Amber Lulu amekanusha kuwa na mahusiano na Nuh Mziwanda.

No comments

Powered by Blogger.