Full-Width Version (true/false)


Anayeniambia mimi nimefulia au sijafanikiwa kimuziki hanijui – Banana Zorro

Msanii mkongwe wa muziki, Banana Ali Zorro amesema kuwa ili msanii apate mafanikio, inatakiwa kwanza awe na ndoto zake alizokuwa amejijengea katika muziki anaoufanya.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Mapenzi gani’, amedai mtu ambaye anamchukulia boa kwenye huu muziki basi atakuwa hamjui vizuri.

“Mtu anayeniambia mimi nimefulia au sijafanikiwa kimuziki, huyo atakuwa hanijui kiundani. Tena na hii lifahamike mimi ndio msanii wa kwanza kuwa na bendi yangu mwenyewe Tanzania na inafanya vizuri. Pia nimeajiri watu katika bendi yangu zaidi ya 20. Nafikiri hayo ni mafanikio makubwa sana kwangu,” Banana Zoro aliiambia MCL Digital.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai amefanya utafiti na kubaini sababu za maisha mafupi ya nyimbo za Bongo Flava, hunasababishwa na kukurupuka kwa wasanii kwa kutoa nyimbo kila kukicha na kujali zaidi maslahi yao kuliko kile wanachowalisha mashabiki wao.

“Unajua ukijali zaidi maslahi, utajikuta unaandaa wimbo mmoja tu wa kibiashara utakaoweza kuwashika mashabiki kila kona, lakini ukikurupuka katika kutoa wimbo utashangaa wimbo hauna meseji yoyote ya maana na unabaki kuwachosha mashabiki zako na kukushusha kiwango,” alisema Banana.

No comments

Powered by Blogger.