Full-Width Version (true/false)


ante amgomea Ngoma Yanga


 

BEKI kitasa wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ anatambua mkataba wake na klabu hiyo upo ukingoni na hatafanya maamuzi ya haraka katika kukimbilia ofa anazopata. Pia amefunguka juu ya kuondoka kwa straika Donald Ngoma akisema aachwe aende zake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Dante alisema Ngoma ni mshambuliaji mzuri ila kusepa kwake Yanga kwenda kutua Azam hakutaiathiri timu yao endapo mabosi wa Yanga watatafuta mshambuliaji mwenye makali zaidi ya Mzimbabwe huyo.
Dante aliyekosa mechi tatu za mwishoni mwa msimu uliofunga pazia jana Jumatatu kufuatia kuugua malaria, alisema anatambua endapo Ngoma atapona na kurejea uwanjani akili yake itataka kuifunga Yanga, lakini haoni kama kazi hiyo itakuwa rahisi kwake kwani wao wanajua wapi pa kumdhibiti.
“Uongozi unatakiwa kutafuta mshambuliaji wa maana zaidi ya Ngoma ili azibe nafasi yake. Akipatikana huyo hata tukutane na timu yenye washambuliaji gani kazi yetu mabeki tutaifanya vizuri na sioni kama walikosea kilichotokea kwa Ngoma kinaweza kunitokea hata mimi, timu haiwezi kusubiri kwa muda mrefu kukosa huduma yako na huku timu haifanyi vizuri,” alisisitiza beki huyo mkali wa mipira ya juu.
     

     

No comments

Powered by Blogger.