Full-Width Version (true/false)


Arsenal yatupwa nje michuano ya EUROPAArsenal imetupwa nje ya michuano ya UEFA Europa Legua kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Atletico de Madrid ya Spain.

Bao hilo pekee limefungwa na mshambuliaji, Diego Costa, katika dakika ya 45 zikiwa zimeongezwa mbili kipindi cha kwanza kumalizika.

Costa amefanya idadi ya mabao kwa Atletico kuwa mawili dhidi ya moja baada ya mechi ya mkondo wa kwanza kwenda sare ya 1-1 huko Emirates na kuifanya itinge fainali ya michuano hiyo.

Mbali na Atletico kushinda, Marseille ya Ufaransa nayo imetinga hatua ya fainali licha ya kufungwa usiku huu kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Salzburg ya Ujerumani na kufanya matokeo hayo yawe 2-3 katika Aggregate.

Marseila iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa huko Ufaransa.

No comments

Powered by Blogger.