Full-Width Version (true/false)


Askari Polisi wajiunga na waandamanaji Ufaransa

Asakari Polisi nchini Ufaransa wamejiunga na waandamanaji katika maandamano ya kupinga siasa za rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.


Askari walikuwa wamejikusanya mbele ya kituo chao cha Polisi wamejiunga na waandamanaji  Paris wanaoandamana kwa muda wa siku kadhaa   wakipinga siasa za rais Emmanuel Macron.


Askari hao wamedai kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu  huku wakikabiliwa na tatizo la mishahara. Vile vile wametoa malalamiko kufanya kazi muda mrefu bila ya kupata muda wa kutosha wa kuwa na familia zao.


Katika maandamano hayo, askari polisi wameomba kuajiriwa kwa askari wapya.


Maandamano hayo nchini Ufaransa kwa sasa yanakaribia kutimiza miezi mitatu tangu kuanza kwake.

No comments

Powered by Blogger.