Full-Width Version (true/false)


Atletico Madrid 'imechoshwa na Barcelona kumnyatia mshambuliaji huyo

Atletico Madrid inasema kuwa imechoshwa na kero la Barcelona la kumnyatia mshambuliaji wake Antoine Griezmann, na imetaka mabingwa hao wa La Liga kuwa na heshima.
Akizungumza siku ya Jumatatu, rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu alisema kuwa alikutana na ajenti wa Griezmann mapema msimu huu

Atletico iliiripoti Barcelona kwa Fifa kuhusu madai ya kumnyatia mchezaji huyo wa Ufaransa mnamo Disemba 27.

"Tumechoshwa na tabia mbaya ya Barcelona ," alisema afisa mkuu mtendaji wa Atletico Miguel Angel Gil Marin.

Marin aliongezea kuwa matamshi ya Bartomeu kuhusu Griezmann kabla ya mechi ya fainali ya ligi ya Europa kati ya Atletico na Marseille mnamo Mei 16 ilionyesha ukosefu wa heshima

Pia aliishutumu Barcelona kwa kuendelea kumshinikiza Griezmann msimu wote huu na kusema kuwa alimwambia Bartomeu miezi kadhaa iliopita kwamba tabia hiyo mbaya ni kinyume na maadili ya La Liga , wakati ambapo timu zote mbili zinapigania taji la ligi hiyo.

Barcelona ilishinda taji la ligi baada ya kuilaza Deportivo La Coruna mwezi uliopita na sasa imebakisha mechi tatu pekee kumaliza msimu bila kushindwa huku Atletico ikiwa katika nafasi ya pili.

Mnamo mwezi Januari, Barcelona ilikana madai kwamba iliuwa imekubaliana na Griezmann ambaye anahudmia kandarasi yake hadi 2022 msimu huu .

"Msimamo wa Atletico Madrid upo wazi na umewekwa wazi mara kadhaa kwamba hakuna hata siku moja tumefanya majadiliano kuhusu Griezmann na wala hatuna nia ya kufanya hivyo'', alisema Marin.'

Aliongezea kuwa awali alikuwa amemuonya Bartomeu kwamba Atletico watadai fidia kutokana na "tabia zisizofaa" za Barcelona iwapo Griezmann atajaribu kuuvunja mkataba wake kutokana na shinikizo kutoka kwa Barca.

No comments

Powered by Blogger.