Full-Width Version (true/false)


Auwa familia yake akidai shamba


Jeshi la Polisi katika Wilaya Kalungu nchini Uganda, linamshikilia kijana Matia kalimunda (22), kwa tuhuma za kumuua mama na kaka yake akidai shamba alilotaka apewe kama sehemu ya urithi wake. 

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa, tukio hilo limetokea leo Mei 31, 2018 katika eneo la Bukulula ambapo mtuhumuiwa alienda nyumbani na kumuua kaka yake Musatafa Gwalamubisi, na kisha kumpiga na jembe mama yake, Bena Nalwadda (80) baada ya kugundua ameshuhudia tukio hilo.

Wakazi waliwasili katika eneo la tukio na kuanza kumshambulia Matia lakini baba wa mtuhumiwa aliyelijulikana kwa jina la Vincent Kasolo, alitokea kwa nia ya kutaka kumtetea mwanae na ndipo wananchi wakamgeuzia kibao na kuanza kumshambulia hadi kupelekea kifo chake.

Msemaji wa Jeshi la Polisi katika eneo hilo Lameck Kigozi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa miili ya marehemu wote watatu imelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Masaka kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Mtuhumiwa wa mauji, Matia Kalimunda amelazwa katika Hospitali hiyo ya Masaka akifanyiwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

No comments

Powered by Blogger.