Full-Width Version (true/false)


Aveva, Kaburu mambo bado magumu mahakamani


 

KESI inayowakabili vigogo wa klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, imeshindwa kusikilizwa na kuahirishwa baada ya Hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na udhuru.
Mbali ya akina Aveva, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na mfanyabiashara Franklin Lauwo, ambao bado hawajakamatwa na juhudi za kuwafatuta ili waunganishwe zinaendelea.
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, jana Jumatatu alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Matha Mpanze, wakati shauri hilo lilipofikishwa kwa ajili ya uamuzi.
Alidai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi, kama ina uwezo wa kumuondoa mshtakiwa wa tatu na wanne katika kesi hiyo au la.
Swai alidai mshtakiwa wa kwanza Evans Aveva hakufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa.
Mawakili wa akina Aveva, Nehemia Nkoko na Timotheo Wandiba Mei 14, waliomba mahakama itoe amri ya kuwaondoa Hanspoppe na Lauwo ambao hawajakamatwa ili waendelee na usikilizwaji wa mashtaka dhidi ya wateja wao ambao walishasomewa mashtaka.
Hakimu Mpanze aliahirisha Kesi hiyo hadi keshokutwa Alhamisi.

No comments

Powered by Blogger.