Full-Width Version (true/false)


Azam FC yachukua tahadhari kubwaIkiwa imebakia siku moja kwa timu ya Azam FC kushuka katika dimba lake kuvaana na Yanga SC, uongozi wa Azam FC umesema wamechukua tahadhari kubwa kuelekea mtanange huo kwa kuwa hawawezi kuwaona wapinzani wao wabovu kutokana na matokeo yake yaliyopita. 

Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa Azam FC, Jafar Idd Maganga wakati akizungumzia hali ya maandalizi kuelekea mchezo huo na kusema mpaka sasa wapo katika hatua za mwisho za maandalizi huku lengo lao kubwa wakiwa wamejikita katika kuchukua nafasi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2017/18 licha kuwa nafasi hiyo haiwapi faida yeyote ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

"Tumejiandaa vya kutosha na kizuri zaidi wachezaji wote ni wazima ukiondoa majeruhi Daniel na Yakubu na waliobakia wapo tayari kwa mpambano huo.Tunafahamu kwamba Yanga ni klabu kubwa na kongwe hapa nchini lakini huu ni mchezo wa mpira huwa unaamuliwa dakika 90", amesema Maganga.

Pamoja na hayo, Maganga ameendelea kwa kusema "lakini sisi kama Azam FC tumechukua tahadhari kwamba Yanga hawakuwa na matokeo mazuri katika michezo yake iliyopita ya hivi karibuni kwa hiyo haitufanyi sisi kuiona Yanga ni timu mbovu au msimu huu sio nzuri.

No comments

Powered by Blogger.