Full-Width Version (true/false)


Azam FC yakusudia kuipoteza Yanga SCUongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC umefunguka na kudai watatumia ipasavyo mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga ili waweze kuchukua ushindi wa nafasi ya pili ambayo kwa sasa ndio nafasi pekee iliyobakia inaangaliwa kwa vilabu hivyo.
 

Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa Azam FC, Jafar Idd Maganga wakati akizungumzia hali ya maandalizi kuelekea mchezo huo na kusema kwa sasa wachezaji wake wote wameingia kambini rasmi Chamazi ambapo watakuwa wanafanya mazoezi pamoja na kulala hapo hapo kwa lengo la kujiweka vizuri kwa mpambano huo.

"Tumeuchukulia mchezo huu kwa uzito mkubwa sana kwa maana tunataka ushindi wa nafasi ya pili lakini nafasi hiyo hatuwezi kuipata kama hatutofanya vizuri katika mechi ambazo zipo usoni kwetu. Yanga kiukweli hawakuwa na matokeo mazuri katika kipindi hiki kwa maana mechi zake za mwisho imekuwa inapoteza poteza lakini Azam FC haitakuja kwenye sura ile ambayo watu wanaiona sasa hivi", amesema Maganga.

No comments

Powered by Blogger.