Full-Width Version (true/false)


Azam FC yamwondoa nyota wa kimataifaMshambuliaji Mghana, Bernard Arthur amevunjiwa mkataba na klabu ya soka ya Azam FC,  baada ya kucheza nusu msimu tu kwenye kikosi hicho huku akishindwa kuonesha makali pengine tofauti na timu ilivyotarajia. 
Nyota huyo alianza vizuri aliposajiliwa Azam FC baada ya kufunga mabao katika baadhi ya mechi zake za mwanzo lakini baadae akaanza kupoteza nafasi chini ya kocha Mromania Aristica Cioaba.

Baada ya kuondolewa kikosini kwa kocha huyo ndio na Artur akafika kikomo kwenye timu hiyo ambapo kocha msaidizi idd Cheche alitoa kipaumbele kwa washambuliaji chipukizi kama Idd Kipagwile na Shaban Idd Chilunda.

Arthur mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao sita katika mechi zake tano za mwanzo akiwa na Azam FC kabla ya kupotea siku chache baada ya kuanza kukaa benchi.

Mghana huyo alisajiliwa Januari mwaka huu kwenye dirisha dogo akitokea Liberty Professionals, kwa mkataba wa miaka miwili, akichukua nafasi ya Mghana mwenzake, Yahya Mohammed ambaye naye aliyevunjiwa mkataba

No comments

Powered by Blogger.