Full-Width Version (true/false)


Azam waeleza sababu zilizopelekea Pluijm kutotangazwa mapema

 
Uongozi wa klabu ya Azam FC umefunguka kwa kuweka wazi sababu zilizowafanya wachelewe kumtambulisha Kocha wao mpya, Hans van der Pluijm aliyerithi mikoba ya Mromania, Aristica Cioba.


Kupitia Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jaffer Idd Maganga, ameeleza kuwa waliamua kufanya hivyo ili kukamilisha taratibu za kumalizana na Pluijm pamoja na mabosi wake wa Singida United.


Maganga amesema watu wengi walikuwa wana haraka ya kutaka atambulishwe mapema na kusahau kuwa kuna taratibu maalum zinazopaswa kufuatwa.


Tayari Azam FC wameshamalizana na Mholanzi huyo anayesubiriwa kumaliza kibarua chake na Singida United cha michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo keshokutwa Jumamosi inacheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali.


Mapema baada ya mchezo huo kukamilika, Pluijm atasafiri kuelekea jijini Dar es Salaam kuja kuanza rasmi kazi ya kuinoa Azam kwa maandalizi ya msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.