Full-Width Version (true/false)


Azam yashika nafasi ya pili VPL,ni baada ya kuifunga Yanga 3-1
Hatimaye mashindano ya ligi kuu ya Vodacom tanzania bara yamefikia tamati leo May 28,2018 kwa mchezo wa mwisho uliowakutanisha Yanga vs Azam fc katika uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ambao ulikuwa na presha kubwa kwa timu zote mbili ikiwa ni wa kuamua  mshindi wa pili umemalizika kwa Azam Fc kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.

Kwa matokeo hayo sasa Azam imechukua nafasi ya pili ya VPL ikiwa na alama 58 nyuma ya mabingwa Simba wakati Yanga imeshika nafasi ya tatu ikiwa na jumla  ya alama 52.

Timu za Majimaji Fc na Njombe mji tayari zimejikatia tiketi ya kushiriki mashindano ya ligi daraja ya kwanza baada ya kushuka daraja kutoka ligi kuu. 

Na huu ndiyo msimamo wa mwisho  wa vpl kwa msimu wa 2017/18

No comments

Powered by Blogger.