Full-Width Version (true/false)


Azam yatoa mapumziko, Simba kusafiri kikaziBaada ya ligi kuu soka Tanzania bara, msimu wa 2017 kufikia mwisho Mei 28, timu mbalimbali zimetoa mapumziko kwa wachezaji wake ikiwemo Azam FC, lakini kwa upande wa Mabingwa Simba wao wanasafiri kikazi. 

Kikosi cha Azam FC kimepewa mapumziko ya siku 35, ambapo wachezaji watakuwa likizo na waterejea kazini rasmi Julai 3 kwaajili ya kuanza maandalizi ya msimu wa 2018/19. 

Wakati Azam FC wakitoa mapumziko hayo, kikosi cha Simba chenyewe kitaendelea na majukumu ndani ya timu ambapo kesho kinatarajia kusafiri kuelekea nchini Kenya, tayari kwa michuano ya SportPesa Super Cup.

Tayari klabu ya Azam FC imeshaweka wazi ratiba yake ya 'Pre-season' ambapo baada ya wachezaji wote watakaosajiliwa na waliopo sasa kurejea watafanya maandalizi kidogo hapa nchini kisha wataelekea nchini Uganda kucheza mechi mbalimbali kwaajili ya maandalizi.

Msimu ujao Simba watakuwa wanashiriki mashindano matatu tofauti, ambayo ni Ligi kuu, Klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho nchini. Azam FC wao watashiriki ligi kuu pamoja na Kombe la Shirikisho.

No comments

Powered by Blogger.