Full-Width Version (true/false)


Baada ya figisu figisu kwenye YouTube, video ya ‘Mvumo wa Radi’ ya Alikiba yarudi kwa kishindo

 

Kwa mashabiki wa Alikiba na wadau wa muziki wa Bongo Fleva kwa siku mbili mfululizo msanii huyo amekuwa akilalamika kuwa video yake ya ‘Mvumo wa Radi’ imefanyiwa figisu figisu kwenye mtandao wa YouTube, hatimaye tatizo hilo kwa sasa limeisha na ngoma hiyo inaendelea kukimbiza mtandaoni.

Kwa siku ya jana asubuhi katika hali isiyo ya kawaida video ya wimbo huo ilipotea ghafla kwenye Trending ya video zinazotazamwa zaidi Tanzania na hadi inapotea kwenye Trending ilikuwa na views 860+k .

Lakini baada ya masaa matano ikarudi tena namba moja kwenye Trending ikiwa na zaidi ya views milioni 1.1 na mpaka sasa video hiyo ina views milioni 1.3 .

Alikiba akizungumza kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM jana Mei 15, 2018 amesema kwa sasa suala hilo limeshafanyiwa ufumbuzi na amewataka mashabiki wake waendelee kufurahia muziki mzuri.

No comments

Powered by Blogger.