Full-Width Version (true/false)


Baada ya kupewa onyo kali,Haji Manara aiomba radhi TFF
Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameliomba radhi Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) kupitia Bodi ya Ligi kufuatia kupewa onyo la kushangilia ndani ya Uwanja katika mechi dhidi ya Yanga.

Manara alishuka kutoka jukwaani na kuingia ndani ya Uwanja baada ya kushindwa kuvumilia furaha aliyokuwa nayo kutokana na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameomba radhi kwa bodi ya ligi huku akieleza kuwa alipitiwa na mhemko baada ya furaha kuzidi.

Licha ya kuomba msamaha huo, Manara ameeleza kuwa hajajua Simba kama ikitwaa ubingwa hali ya furaha yake itakuwaje, yawezekana akaingia tena Uwanjani kushangilia na kucheza.

"Muungwana akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa mshabiki kama kumgalagaza mtani...it will never happen again..ila sijui itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwali😁😁😁 @tanfootball #bodiyaligi πŸ™πŸ™".Ameandika Haji Manara
 
Mapema leo mchana Bodi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi kupitia Mwenyekiti wake Clement Sanga ilitoa onyo kali kwa Manara, kuhusiana na kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Kitendo cha kufanya hivyo ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

No comments

Powered by Blogger.