Full-Width Version (true/false)


Baada ya kupiga Hat-Trick, Lionel Messi ajihami kuelekea Kombe la Dunia nchini UrusiJana usiku mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa Argentina, Lionel Messi ametupia goli tatu kati ya nne zilizotupiwa na Argentina kwenye mchezo wao kirafiki dhidi ya Haiti.

Messi ambaye ndiye aliyeibuka ‘Man Of The Match’ kwenye mchezo huo amesema kuwa ni mchezo wa kujipima nguvu na kujiimarisha kuelekea kombe la dunia lakini matokeo hayo sio picha kuwa timu yake ipo vizuri kuliko zingine.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona, amedai kuwa mafanikio ya timu hayaletwi na mtu mmoja, hivyo ni lazima wachezaji wote kwa pamoja wajitume uwanjani hii ni baada ya watu wengi kumuangalia mchezaji huyo kama tegemeo kwa timu ya taifa ya Argentina.

Timu zote zinaenda Urusi zikiwa na lengo moja la kurudi na ushindi, Kombe la Dunia ni ndoto yetu na kwa taifa kwa ujumla. Sisi ni moja ya timu ambazo hazifikiriwi kuchukua kombe. Kama nilivyowahi kuwambia siku za nyuma, mafanikio ya timu yoyote hayaletwi na mtu mmoja, hii ni kutokana na aina ya mpira wa kisasa wa siku hizi. Najua tuna wachezaji wazuri na kwa sasa tunaanza kuelewana,“amesema Messi na kusisitiza.

Kwa sasa macho yetu yapo kwenye kombe la dunia, na tunachohitaji ni kushinda mchezo wetu wa kwanza ili tupunguze presha na kisha kushinda mechi zote zitakazokuwa zimesalia.“amesema Messi.

Argentina mwaka 2014, walichabangwa goli 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia je, mwaka huu watafika fainali tena?

No comments

Powered by Blogger.