Full-Width Version (true/false)


BAADA YA TFF KUTUMA BARUA WIZARANI IKIOMBA RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI SIMBA KOMBE, KIONGOZI WA MATAWI YANGA AFUNGUKA


Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Rais wake, Wallace Karia, kutuma maombi Wiazara ya Michezo likiomba ugeni rasmi kutoka kwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi mechi ya Simba dhidi ya Kagera, Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini, Bakili Makele afunguka.
Makele ameeleza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini pamoja na Yanga kwa ujumla hawana kinyongo na suala hilo kutokana na ombi hilo la TFF kumuhitaji Rais Magufuli awe mgeni rasmi.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakielezwa kuwa Yanga imepatwa na kinyongo sababu bingwa wa nchi amekuwa Simba, jambo ambalo amesema si sahihi.
Makele amefunguka kwa kueleza Simba ndiye bingwa wa nchi kwa sasa na wanastahili pongezi kutokana na kazi kubwa waliyoifanya msimu huu.
Aidha, Makele ameipongeza serikali na Rais Magufuli endapo atahudhuria katika mchezo wa Simba na Kagera ambao utakuwa na hafla ya kuwakabidhi Simba taji la ligi Mei 19 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.
Mbali na Simba, Magufuli atawakabidhi Serengeti Boys Kombe la CECAFA (U17) walilolitwaa huko Burundi kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

No comments

Powered by Blogger.