Full-Width Version (true/false)


Barnaba awakana wapenzi wake wote


 Mwalimu na mwanamuziki wa bongo fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amesema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yoyote, huku akidai endapo siku ataamua kuweka wazi juu ya mahusiano yake basi watu wafahamu kuwa anaoa ama anamvalisha pete ya uchumba mpenzi wake nasio vinginevyo. 
Barnaba ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya picha zake kuzagaa  kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea baadhi ya watu kudai huwenda wanawake hao anatoka nao kimapenzi nasio vinginevyo.

"Sijui chochote kinachoendelea, nilisema siku ambayo nitakuja kumtangaza mwanamke wangu basi kuna mawili naoa au namvisha pete ya uchumba kwa hiyo sina mapenzi ya mitandao sana na mpenzi wangu nimpendae kwa kweli siwezi kumuweka kwenye mitandao, mwanamke wangu ninamuheshimu  na nitakaye kuja kumpa nafasi ya maisha si mwanamke atakayekuja kuwa wa mitandaoni kiukweli sidhani kama mwanamke wangu anatakiwa kuwa kwenye chombo cha maonesho ya mitandao", amesema Barnaba.

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Barnaba tayari ni 'star' na watu wakiniona nipo nimesimama na mwanamke huyu mara yule wanahisi labda ni wapenzi wangu. Mimi sina mwanamke wala mpenzi 'of course am gentleman' muda mwingine nina haja zangu ninajua namna gani ninavyozikidhi lakini sina makubaliano ya aina yeyote ya kimapenzi kama kijana kusema kwamba hapa nimefunga".

No comments

Powered by Blogger.