Full-Width Version (true/false)


Ben Pol apondwa kisa vazi lake

Benard Paul ‘Ben Pol’

MWANAMUZIKI anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, Benard Paul hivi karibuni amefungukia mashuti aliyopewa na mashabiki wake baada ya kuposti mtandaoni akiwa amepozi huku ametupia vazi lenye fasheni ya kuchanikachanika.

Akipiga stori na Over Ze Wekend, Ben Paul wimbo wake aliomshirikisha uitwao Zai, aliomshirikisha Kiss Daniel unafanya vizuri, alisema wanaomponda ni watu wasiofahamu masuala ya fasheni.

“Ile ni nguo yangu tu ya siku nyingi na nilivaa ikiwa safi ila watu wasiyofahamu masuala ya fasheni walikuwa wanaponda. Umefika wakati Wabongo wanatakiwa wabadilike na kufahamu fasheni zinakuwa na hazibaki palepale walipokuwa wanafahamu wao,” alisema Ben Pol.

No comments

Powered by Blogger.