Full-Width Version (true/false)


Benzema amshangwazwa Rais wa Shirikisho la soka Ufaransa

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema ameshangazwa na kitendo cha Rais wa Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF), Noel Le Graet kumuongelea kwenye vyombo vya habari.


Benzema hajachezea timu ya taifa ya Ufaransa tangu mwaka 2015 alipocheza dhidi ya Armenia kufuatia madai ya kutatanisha ya kutishia maisha yaliyomuhusisha mchezaji mwenzake, Mathieu Valbuena.


Licha ya kiwango chake kizuri akiwa na vigogo wa Hispania kwa miaka yote hii, Benzema amekuwa akifungiwa vioo na kwa mara nyingine anakosekana kwenye kikosi cha Kombe la Dunia Urusi.


Na Rais wa FFF, Le Graet, ambaye miaka ya nyuma alikuwa mmoja wa watetezi wakubwa wa Benzema, sasa ameweka wazi kwamba kikosi lazima kisonge mbele bila yeye.


"Hii ni hadithi ya zamani, na hatuwezi kurudi nyuma," amefafanua kwenye L'Equipe.


"Kila mmoja anakubali kwamba ni mchezaji mkubwa, wakati wote anaanza na Real Madrid, lakini kwa France, ni sehemu ya historia. Timu yetu sasa ina staili fulani, na hatuwezi kurudi nyuma katika hilo,".


Na baada ya kusikia nukuu hizo, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akaenda kujibu kwenye ukurasa wake wa Twitter.


Benzema amesema: "Bw. Graet, kwa heshima zote, umepoteza fursa ya kubaki kimya. Nimeijua sura yako halisi, na huyu si yule aliyesema ananikubali mimi na asingeweza kujadili uteuzi wa timu,".

No comments

Powered by Blogger.