Full-Width Version (true/false)


Bilionea wa Chelsea Roman Abramovich apewa uraia Israel baada ya kutoswa Uingereza


Mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, bilionea mwenye asili ya Urusi, Roman Abramovich amepewa uraia wa nchini Israel.


Imedaiwa kuwa Abramovich amefikia maamuzi ya kuhamia Israel baada ya Uingereza kumcheleweshea kumpatia Visa katika kinachoonekana kilichochangia zaidi ni mzozo wa kidplomasia uliopo kati ya Uingereza na Urusi.

Mzozo huo uliibuka March 4 mwaka huu baada ya jasusi wa Urusi, Sergei Skripal na binti yake Yulia Skripal kupewa sumu.

Gazeti la The Times Israel limeripoti kuwa Abramovich amewaili nchini humo Jumatatu hii kwa ajili ya kuweka makazi yake mapya.

Abramovich anatajwa kuwa anaweza akawa ndio tajiri zaidi nchini Israel sasa.

No comments

Powered by Blogger.