Full-Width Version (true/false)


Bilioni 1.2 zatolewa kwaajili ya wananchi

Serikali imemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya kufuatilia shilingi Bilioni 1.2 za kulipa fidia wananchi, watakaopitiwa na mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa shilingi bilioni 476 ili usikwame kutekelezwa. 
Akitoa agizo hilo Mei 28, 2018 Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya AUWSA, na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Dkt. Isack Kamwelwe na kusema fedha hizo zipo tayari na kinachotakiwa kufuatiliwa ili wiki hii zipatikane na mradi uendelee.

"Mradi huo ukitekelezwa utapunguza uhaba wa maji ambao kwa sasa yanapatikana kwa asilimia 44, ambayo hayatoshi wakazi zaidi ya laki tano hivyo kupitia mradi huu unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) itafanikisha maji kupatikana kwa asilimia 100 siku za karibuni", amesema Mhandisi Kamwelwe.

Pamoja na hayo, Mhandisi Kamwelwe ameendelea kwa kusema "lengo la kutoa fedha za fidia ni kuwezesha mradi kufanikiwa kwa wakati, japo umecheleweshwa kutokana na sababu za ulipwaji fidiana zingine".

Aidha, Mhandisi Kamwelwe amesema katika utekelezaji wa mradi huo, muhimu kuzingatia suala

la kupanua mtandao wa maji taka, ambalo kwa sasa linatiliwa mkazo na baadaye lazima kuwe na Sera na sheria ya maji taka, ili mwisho wa siku baada ya matumizi ya maji safi yatumike vizuri ili kuepuka uharibifu wa mazingira.


Kwa upande mwingine, Mhandisi Kamwelwe amesema atahakikisha miradi ya maji inayotekelezwa nchini kwa gharama kubwa inafikiwa lengo husika huku akiunda kamati ya uchunguzi wa miradi yote ya maji nchini ambayo itapita kila Mkoa.

No comments

Powered by Blogger.