Full-Width Version (true/false)


Bill Nas akiri kuwa mwizi
Rapper ambaye anafanya poa kwenye game la bongo Bill Nas, amekiri kuwahi kuwa mwizi kwenye maisha yake, na kufanya matukio mbali mbali. 
Bill Nas amefunguka hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI East Africa Television, na kueleza kwamba alipokuwa mtoto kuna vitu alikuwa anavihitaji lakini alikuwa hana namna ya kuvipata zaidi ya kuiba, huku akipata shinikizo kubwa kutoka kwa makundi aliyokuwa nayo.

“Nimeshawahi kuiba siwezi kudanganya katika hilo, sijawahi kufanya wizi mkubwa, lakini nishawahi, unajua hii inatokea pale labda tunahitaji kitu fulani, halafu tunajua tunakipata sehemu fulani, ila ni utoto, kipindi hiko niko shule ya msingi ndiyo nilikuwa na makundi ambayo hayafai”, amesema Bill Nas.

Rapper huyo ameendelea kwa kusema kwamba pia malezi ambayo ameyapata kutoka kwa baba yake ambaye ni 'mzee kijana, yamempelekea kuwa mtoto ambaye alikuwa akifanya mambo mengi yasiyofaa.

No comments

Powered by Blogger.