Full-Width Version (true/false)


Bocco ajivunia rekodi yake Simba 

Baada ya mshambuliaji John Bocco kucheza kwa mafanikio makubwa katika msimu wake wa kwanza Simba, amefichua siri ya kamati ya usajili ya klabu hiyo, ilisajili mastaa wa maana.
Bocco anasema bila kuwa na kikosi kizuri, anaamini isingekuwa rahisi kufikia hatua ya ubingwa na kutoa mfungaji bora na wa pili.
"Ulikuwa ni msimu wa kihistoria kwetu, bila shaka hiki kikosi hakitasahaulika kama ilivyo kwa kocha Abdallah Kibaden ambaye alifunga Hatrick dhidi ya Yanga inayokumbukwa mpaka sasa, kwetu tumechukua ubingwa, mfungaji bora na wapili," anasema Bocco.
Pamoja na mafanikio hayo, Bocco anasema hawawezi kujibweteka kwa kufanya mazoezi binafsi wakiandaa miili yao kwa ajili ya michuano ya kimataifa, mwakani.
"Nimejifunza kwa wenzetu huwa wanafanya maandalizi ya muda mrefu na ndio maana unakuta wapo fiti muda wote, binafsi hata nikipata mapumziko haina maana kwamba basi nitajibweteka la bali nitakuwa na programu zangu za mazoezi," anasema Bocco.

No comments

Powered by Blogger.