Bulaya, Halima Mdee Wakwama Kufika Mahakamani
Wabunge
Esther Bulaya pamoja Halima Mdee ambao ni washtakiwa katika kesi ya
jinai namba 112 ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko
usio halali kinyume cha sheria wameshindwa kufika mahakamani leo
kutokana na usafiri waliokuwa wakitumia kupata matatizo.
Hayo
yamebainishwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa sababu ya washtakiwa hao kutokuwapo
mahakamani imetokana na usafiri waliokuwa wanatumia kutoka bungeni mjini
Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuwa na tatizo na kusababisha wachelewe
kufika.
Katika
kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabili viongozi tisa
wa CHADEMA, akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe Halima Mdee
, ni mshtakiwa wa saba, na Ester Bulaya ni mshtakiwa wa tisa.
Mbali
na Bulaya pamoja na Mdee washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji , Mbunge wa Iringa Mjini Mch.
Peter Msigwa, Naibu makatibu wakuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na John
Mnyika (Bara), Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko, na Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche.
Viongozi
hao wa CHADEMA wanakabiliwa na mashtaka 12 katika hiyo ya kufanya
mkusanyiko na maandamano yasiyo halali Februari 16, 2018
yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.
No comments