Full-Width Version (true/false)


Bulembo: Nimeacha akaunti ikiwa na TZS 2.2 Bilioni na rekodi yangu haiwezi kuvunjwa
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba amehusika na ufisadi wa mali za jumuiya hiyo hazina ukweli.


Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Mei 29, 2018 Bulembo amesema vikao vya CCM vilivyoanza jana vitatoka na majibu sahihi.


“Nimefanya kazi CCM kwa utiifu na heshima kubwa. Hadi naondoka nimeacha Sh2.2 bilioni katika akaunti, rekodi hii haiwezi kuvunjwa,” amesema Bulembo ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa .


Amesema vikao vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM vinavyotarajiwa kumalizika leo vitakuja na majibu yatakayowaumbua wanaomtuhumu kupitia ripoti ya uchunguzi wa mali za CCM iliyofanywa na kamati iliyoundwa na mwenyekiti wa chama hicho tawala, Rais John Magufuli.

No comments

Powered by Blogger.