Bunge: Si Lazima Kutoa Video Za Wabunge
Naibu
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema Kitengo cha Habari cha Bunge
hakilazimishwi kutoa taarifa za video za wabunge zinazorekodiwa wakati
wakichangia mijadala mbalimbali ndani ya Bunge hilo.
Dk.
Tulia ametoa kauli hiyo leo Mei 9, wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa
Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), aliyehoji nani anayetoa amri
kwa kitengo hicho kukata kwa asilimia 90 maelezo ya video za wabunge
wanaochangia mijadala mbalimbali bungeni.
Lijualikali
amesema licha ya kwamba wabunge wanaongozwa kwa kanuni kuzungumza na
hakuna amri ya kufuta kauli unayozungumza bungeni hadi mwisho
inashangaza kuona kwenye vipande vya video wananyimwa au inakatawa.
“Unapewa
‘hansard’ iliyokamilika, lakini cha ajabu watu hao wa hansard
tunapoenda kuomba video zetu ambazo tumeongea humu bungeni, zinakuwa
zimekatwa kwa asilimia 90 hawa wanaokata hotuba zetu wanakata kwa amri
ya nani, wakati mbunge nimeongea na kiti kimeniruhusu niongee hadi
nimemaliza, anayekata, anakata kwa amri ipi na kwa maelekezo ya nani,
naomba mwongozo,” amesema.
Akijibu
mwongozo huo, Dk. Tulia alisema taarifa rasmi za Bunge huchapwa na
mbunge kukabidhiwa, lakini utaratibu wa bunge kutoa clip za wabunge
hiyo hutegemea utashi wa kitengo cha habari.
“Kwa
hiyo kuna wakati wanaweza wasikupe na hawalazimiki kufanya hivyo, kwa
hiyo kama kuna jambo lolote ambalo umeenda kuomba na hawajakamilisha
waambie unaomba muda wako wa dakika 10 kama labda wamekupa dakika mbili
badala ya 10 waambie unahitaji zote.
“Sasa
inategemea ninyi mmetumia utaratibu upi kuzipata hizo taarifa lakini
taarifa rasmi za Bunge ni zile zilizoandikwa na si hizi tunazozungumza.
Huo ndiyo utaratibu tulio nao,” amesema.
No comments