Full-Width Version (true/false)


CAF yairuhusu Yanga kutumia jezi za sportpesa


Shirikisho la soka Barani Africa CAF limeipa ruhusa klabu ya Yanga kutumian jezi zake zenye nembo ya wadhamini baada ya kuwawekea zuio kwenye mchezo dhidi ya U.S.M Alger wikiendi iliyopita.

Taarifa ya Klabu ya Yanga iliyotolewa jioni hii imeeleza kuwa, baada ya wao kuliandikia barua shirikisho hilo limewajibu kuwa wapo huru kutumia jezi zao hizo ambazo wamekuwa wakizitumia msimu huu wote.

''Rasmi, CAF wameiruhusu Yanga kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu wa timu Sportspesa kwenye mechi zake za hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Africa'', imeeleza taarifa hiyo.

Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza wa makundi jumapili iliyopita na kukubali kichapo cha mabao 4-0 ugenini. Katika mchezo huo Yanga walilazimika kutumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini.

Mchezo unaofuata wa Yanga kwenye hatua ya makundi utachezwa Mei 16 jijini Dar es salaam wakiwaalika Rayon Sport ya Rwanda na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.

No comments

Powered by Blogger.