Full-Width Version (true/false)


CAF yamfungia nyota wa YangaKuelekea mchezo wa kesho wa Kombe la shirikisho Barani Afrika kati ya wawakikishi wa Tanzania Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, kiungo wa Yanga Said Juma Makapu hatakuwa sehemu ya mchezo huo. 
Yanga imethibitishsa kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, ambazo kwa mujibu wa kanuni za CAF anatakiwa kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

Makapu alipata kadi hizo mbili mfululizo kwenye mechi mbili zilizopita akianza na ile ya mtoano kati ya Yanga na Welayta Dicha ya Ethiopia, kabla ya kupata tena kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya U.S. Alger.

Mchezo wa kesho ni wa pili kwa Yanga katika hatua ya makundi ambapo itakuwa inasaka ushindi ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa Kundi D, lenye timu za U.S.M Alger, Gor Mahia, Rayon Sports na Yanga wenyewe.

Hadi sasa msimamo wa kundi hilo unaongozwa na U.S.M Alger ambao walipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Yanga, huku Gor Mahia na Rayon Sports wakiwa wa pili na tatu baada ya sare yao ya 1-1. Yanga inashika nafasi ya mwisho ikiwa haina alama.
 

No comments

Powered by Blogger.