Full-Width Version (true/false)


Chakula chadhibiti utoro shuleni

 Wilaya ya Mkinga imesema toka waanze mpango wa kutoa chakula cha mchana shuleni utoro umepungua kwa wanafunzi licha ya kwamba bado kuna wazazi ambao hawajawa  na uelewa wa jambo hilo. 
Afisa elimu wa halmashauri hiyo Zakayo Mlenduka amesema jambo hilo limefanikiwa baada ya kuzishirikisha serikali za vijiji kuwabana wazazi kuchangia chakula cha watoto wao wakiwa shuleni.

Pamoja na hayo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, amesema katika kufanikisha jambo hilo wamezitaka shule za msingi kuwa na mashamba ambayo watalima mahidi na mazao mengine kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wao.

No comments

Powered by Blogger.