Full-Width Version (true/false)


Chanjo haiwezi kuwa msaada- Daktari


 


Chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi imeelezwa kuwa haitokuwa na msaada endapo mtoto atakuwa ameshiriki tendo la ndoa na kupata maambukizi hayo akiwa na umri wa miaka 14. 
Maambukizi ya ugonjwa huo yanatokana na kujamiiana, ambapo wakati huo huo vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike vinaripotiwa nchini ikiwemo kubakwa na kulawitiwa katika umri mdogo.

Eatv.tv ilimtafuta Daktari ili kupata ufafanuzi endapo mtoto aliwahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia itakuwaje?.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dk. Festo Dugange amebainisha kuwa pamoja na kupatiwa chanjo hiyo lakini endapo mtoto atakuwa tayari amepata maambukizi hayo, chanjo haitakuwa na msaada kwake.

“Maambukizi ya ugonjwa huo yanatokana na ushiriki wa tendo la ndoa kwa mtoto wa kike na tumechagua umri huo kwakuwa kwa mujibu wa makadirio muda huo motto wa kike anakuwa bado hajaanza lakini endapo ikitokea motto alitendewa ukatili na akapata aidha kwa kubakwa au la hawezi kusaidiwa na chanjo hiyo kwakuwa tayari atakuwa na maambukizi tayari”, Dkt. Festo.

Saratani ya mlango wa kizazi imetajwa kuwa inaongoza kusababisha vifo kwa asilimia 32.8 kwa akina mama nchini.

No comments

Powered by Blogger.