Full-Width Version (true/false)


Cr7 ampasua mpiga picha wakati wa “kutest mitambo”

Leo ni leo asemaye kesho ni muongo, leo ni ama Mo Salah abebe Champions League yake ya kwanza au Cristiano Ronaldo abebe Champions League yake ya tatu mfululizo lakini hata iweje mshindi lazima apatikane.

Tayari timu zote ziko mjini Kiev ambapo ndio mji fainali hizi zitapigwa, vikosi vyote viwili kile cha Liverpool na kile cha Real Madrid wameshafanya mazoezi ya mwisho mwisho kuelekea katika mtanange huu.

Lakini wakati Cristiano Ronaldo akiwa katika mazoezi ya mwisho mwisho amempasua juu ya jicho muandishi mmoja baada ya mpira alikuwa ameupiga shuti kwenda off target na kumpiga muandishi huyo.

Muandishi huyo aliyefahamika kwa jina la Lorenzana Prieto anafanya kazi katika kituo kimoja cha habari ya Hispania kiitwacho Univision Deporters alikuwa katika harakati za kupiga picha ndipo dhahma hiyo ilipomkuta.

Ronaldo alimnyooshea mkono muandishi huyo kumuomba msamaha, na baada ya mazoezi alimtumia jacket yake aliyokuwa amevaa juu kama njia ya kumuomba msamaha muandishi huyo ambaye hata hivyo alionekana fiti baadae huku akiwa na plasta usoni.

Leo mashabiki wa Real Madrid watategemea mashuti kama hayo yawe on target ili kuweza kuimaliza Liverpool, Cristiano hadi sasa ana mabao 15 katika Champions League na anategemewa kuibeba Real Madrid hii leo pia.

No comments

Powered by Blogger.