Full-Width Version (true/false)


DC Tesha atoa tahadhari kwa wanaonunua viwanja
Mkuu wa Wilaya Nyamagana jijini Mwanza Mary Tesha amewataka wananchi wanunuapo viwanja wajiridhishe katika Ofisi ya Ardhi ya Jiji kama eneo hilo ni salama na halali.

Tesha amesema hayo wakati alipokuwa akitatua migogoro ya ardhi katika Kata Mhandu aliwataka wananchi wawe makini wengine wanauziwa mara mbili huku wengine wakiuziwa maeneo ya wazi.

"Baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa sio waaminifu wanajari maslahi binafsi wanasainisha maeneo ambayo ni ya wazi na wengine wakipandilia bei kwa kiwanja ambacho kimeuzwa tayari," alisema.

Pia alitoa rai kwa wananchi wanapotaka kujenga katika viwanja vyao wahakikishe wamepata kibari kutoka Halmashauri inayoonesha aina ya nyumba inayotakiwa kujengwa eneo hilo kulingana na Ramani ya Jiji.

Aidha alisema kuwa Halmashauri ya Jiji inaendelea kuwalipa fidia wananchi ambao  maeneo yao yalichukuliwa na serikali kwa shughuli mbalimbali kijamii ikiwemo maeneo ya vituo vya afya na shule.

No comments

Powered by Blogger.