Full-Width Version (true/false)


Derby ya Mashemeji yaamuru Gor Mahia kuikabili Hull City ya UingerezaKlabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo ni mabingwa mara 16 imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 5 – 4 mbele ya hasimu wake wa kihistoria timu ya  AFC Leopards kwenye mchezo uliyo pigwa hapo jana dimba la Afraha Jijini Nakuru.

Kwenye mchezo huo ambao ulikuwa unaamua nani atacheza na klabu ya Hull City ya Uingereza Mei 13 mjini Nairobi, Gor Mahia imeendeleza ubabe wake wa kutokufungwa na mpinzani wake wa jadi timu ya AFC Leopards kwa michezo miteno sasa baada ya kupata ushindi huo wa mabao 5 – 4 kwa njia ya mikwaju ya penati mara baada ya dakika 90 kumalizika pasipo yoyote kuona lango la mwenzake.

Mgeni rasmi kwenye mchezo huo wa watani wa jadi, Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Raila Odinga na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SportPesa walishuhudia mabingwa mara 13 wa ligi kuu ya Kenya klabu ya AFC Leopards wakipata kipigo kutoka kwa hasimu wao Gor Mahia.

Hull City itashuka dimbani kuikabili Brentford kwenye ligi ya Uingereza Mei 6 klaba ya kuanza ziara yake nchini Kenya kuwakabili Gor Mahia.

Timu ya Gor Mahia itakuwa ni mchezo wake wa pili kucheza na timu za Uingereza baada ya mwaka jana kuwafunga Leopard 3 – 0 fainali ya michuano ya SportPesa Cup na kukata tiketi ya  kuikabili Everton  Jijini Dar Es Salaam na kukubali kipigo na jumla ya mabao 2 – 1.

Hull City si timu ngeni kwa Wakenya kwani timu ya mastaa kutoka Ligi Kuu ya Kenya (SportPesa All Stars) ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye dimba la K-COM nchini Uingereza mnamo Februari 27, 2017.

Hull, Gor na Leopards zinapata udhamini kutoka kwa kampuni ya bahati nasibu ya SportPesa. Mwaka 2016, SportPesa ilitangazwa wadhamini wakuu wa Hull baada ya kusaini kandarasi ya misimu mitatu (2016/17, 2017/18 na 2018/19).

No comments

Powered by Blogger.